
Hayo yamefanyika katika Mkutano wa Baraza uliofanyika kwa siku mbili Mkoani Daresalaam kwa tarehe 29 na 30 mwezi Mei. Katibu Mtendaji kwa niaba ya Menejimenti aliwakabidhi wajumbe nyenzo hizo na kusema kuwa zitawasaidia hata kutumia katika vikao vya kimtandao yaani 'eBoard'. Alieleza kuwa vifaa hiyo vya kisasa vitasaidia pia kupata taarifa za kiuwezeshaji nchini na hata nje ya nchi.
Naye Mwenyekiti wa Baraza Profesa Aurelia Kamuzora kwa niaba ya wajumbe wa Baraza alimshukuru Katibu Mtendaji na Menejimenti yake kwa hatua hiyo kwani dunia ya sasa imekuwa ikkikuwa kwa kasi hasa kwenye sekta ya Teknolojia. Hivy kwa kuwapatia vifaa hivyo vya kisasa kama vitendea kazi kutaenda kurahisisha kazi zao hasa kwenye masuala mazima ya Uwezeshaji.