“Naomba nitoe shukrani zangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza” aliongeza Katibu Mtendaji.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) Bw. Jabiri Makame aliyasema hayo tarehe 13 Novemba,2026 katika hafla ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Midland Dodoma.
Alisisitiza suala la kufanya maamuzi kwa pamoja kwani misingi yake ya kiuongozi ni kuamua jambo kwa pamoja (Collective Leadership) na sio uongozi wa mtu mmoja, kushirikishana katika kila jambo, kupanga, kujadiliana, kupeana ushauri na kukubaliana mwelekeo bora ili Baraza likidhi matarajio yake kwa mujibu wa Sera, Sheria lakini pia likidhi matarajio ya Mhe. Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Alisisitiza kuwa Baraza ni chombo kikubwa kilichopewa mamlaka kwa mujibu wa Sera yake kwa kuwa ndio chombo cha juu kinachohusika na kusimamia, kufuatilia na kuratibu shughuli zote za Iwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Katibu Mtendaji aliongeza kuwa ni jukumu la Baraza kuhakikisha malengo ya kuwawezesha Watanzania yanafikiwa kwa mujibu wa DIRA 2050 na kila Mtanzania aweze kufikia pato la dola 7000 kwa mwaka.
Katibu Mtendaji alisema kuwa kwa muda mfupi ameweza kukutana na viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu SBUU akiwemo Waziri Prof. Palamagamba Kabudi.
“Katika mambo aliyosisitiza Waziri ni uwepo wa mfuko wa Uwezeshaji utakaoweza kuwawezesha Watanzania moja kwa moja. Vilevile uwepo wa Kanuni za jumla za Uwezeshaji zitakazoweza kuliongoza vizuri Baraza na ziwe tayari kabla ya tarehe 30 Novemba” alisema Katibu Mtendaji.
Katibu Mtendaji alimshukuru Mwenyekiti wa Baraza kwa kuweza kuhudhuria hafla hiyo na kuwapongeza wajumbe wa Bodi ya Baraza kwa kulisimamia Baraza.
Nae Mwenyekiti wa Bodi Prof. Aurelia Kamuzora alieleza kuwa maana ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na kusisitiza kuwa Watanzania tunapaswa kutumia Malighafi zinazopatikana nchini na kutumia Kama Fursa ya kukuza Uchumi wetu.
Kaimu Katibu Mtendaji aliyepita Bw. Gwakisa Bapala alimpongeza Bw. Jabiri Omari Makame kwa kuaminiwa na Mhe. Raisi na kumuahidi Ushirikiano kwa muda wote watakaofanya kazi pamoja.
#NEEC Kuimarisha Uchumi wa Wananchi

