KIKAO CHA 11 CHA WADAU WA VIKUNDI VYA KIJAMII VYA HUDUMA NDOGONDOGO ZA KIFEDHA
Imewekwa: 26 May, 2026
KIKAO CHA 11 CHA WADAU WA VIKUNDI VYA KIJAMII VYA HUDUMA NDOGONDOGO ZA KIFEDHA

Baraza la Taifa la Uwezeshaji wa Kiuchumi (NEEC) kimefanya kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa wadau wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogondogo za kifedha (Community Microfinance Groups) wakiwemo Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), CCT, Centre for VICOBA microfinance and Enterprise Development and Community Educator Empowerment Development (CEVEDE-CEED), Shirikisho la Vicoba Tanzania (VIKOBA-FETA), Benki kuu ya Tanzania (BOT) pamoja na Dodoma Jiji.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Midland Hotel mkoani Dodoma, kikilenga kuimarisha ushirikiano na kujadili mikakati ya kukuza huduma ndogo za kifedha kwa wananchi kupitia vikundi vya kifedha vya kijamii.

Washiriki walijadili namna ya kuendelea kuimarisha uwezo wa vikundi vya kijamii katika usimamizi wa huduma ndogondogo za kifedha, kuongeza uelewa wa masuala ya fedha na kuweka mazingira bora ya wananchi kunufaika na fursa za uwezeshaji wa kiuchumi.

Aidha, kikao kilisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za serikali, taasisi za dini na mashirika ya maendeleo katika kuhakikisha vikundi vya kijamii vinaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo

slot gacor