KIKAO CHA 20 CHA KAMATI YA MIFUKO NA PROGRAMU ZA UWEZESHAJI
Imewekwa: 11 Jun, 2026
KIKAO CHA 20 CHA KAMATI YA MIFUKO NA PROGRAMU ZA UWEZESHAJI

KIKAO CHA 20 CHA KAMATI YA MIFUKO NA PROGRAMU ZA UWEZESHAJI
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi Bw. Gwakisa Bapala ameongoza kikao cha 20 cha kamati ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji kilichofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Mkoani Dodoma.
Kikao hicho kimeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) na kimehudhuriwa na Kamati ya Mifuko ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Self Microfinance, Azania Bank,REA, Baraza la Taifa la Michezo, Mfuko wa Taifa wa Maji na mifuko na programu nyinginezo
Lengo la Kikao hicho ni kujadili namna Mifuko hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika kuinua Uchumi wa Wananchi na Taifa kwa ujumla pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha huduma zao kwa kujitangaza zaidi na kufungua fursa nyingi kwa Wananchi.
Katika wasilisho kutoka NEEC Meneja wa Mifuko na Programu za Uwezeshaji Bw. Emmanuel Subbi amewaomba wadau kutoka katika Mifuko iliyoshiriki katika kikao kazi hicho kuandaa taarifa zitakazosaidia katika utekelezaji wa Majukumu yao na kutathmini kazi zinazofanywa na Mifuko hiyo.
Nae Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania kutoka NEEC Bi. Neema Mwakatobe amesema ni wajibu wa mifuko yote ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi kujitangaza zaidi,kutoa elimu kwa wananchi ili kuonesha fursa mbalimbali kwa Wananchi lengo ni kuinua Uchumi wao.
Sambamba na hayo, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Takwimu Bw. Isaac Dirangw alifanya wasilisho kuhusu Mfumo wa Kitaifa wa usimamizi wa Taarifa za Uwezeshaji (NeMIS) kwa wajumbe na kuwaelezea namna utakavyosaidia katika ukusanyaji wa Taarifa kwa njia ya kisasa.
Kaimu katibu Mtendaji wa NEEC ameishukuru kamati ya Mifuko kwa kushiriki vema katika kikao hicho na  kuwataka kutoa ushirikiano kwa NEEC katika utoaji wa taarifa za Mifuko hiyo ili kurahisisha mchakato wa taarifa hizo.
Kikao hiki cha 20 cha Kamati ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji ni muendelezo wa vikao vinavyofanyika kila mwaka inayowakutanisha kamati ya Mifuko lengo kubwa likiwa nikujadili  tathmini ya maendeleo ya Mifuko yote ya Uwezeshaji na kuweka mpango mkakati wa kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa katika Mifuko ya Uwezeshaji ili kuinua Uchumi wa Taifa.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo

slot gacor