KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI NEEC CHAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 6,886,563,650 KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kimepitisha bajeti ya kiasi cha Shilingi Bilioni6,886,563,650 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Haya yamefanyika katika Ukumbi wa Lush Garden uliopa Arusha. Kikao hicho kimeongongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza Ndg. Gwakisa Bapala, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Ndg. Samwel Nyungwa, mwakilishi wa TUGHE Taifa Ndg. Tamsoni Mshighati wajumbe wa Baraza.
Akifungua kikao hicho Kaimu Katibu Mtendaji alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ongezeko la bajeti kwenye Taasisi kuanzia Julai 2025.
"Nichukue nafasi hii kwa kuwapongeza kwa kufika kwenye kikao hiki na wafanyakazi wote wawe huru kutoa maoni na sisi kama menejimenti tutayachukua yale yote ya msingi na kuyafanyia kazi" aliongeza Kaimu Katibu Mtendaji.
Naye Katibu wa TUGHE Mkoa, alilipongeza Baraza kwa kikao kizuri na kuahidi kuendelea kutoa Ushirikiano kwa Baraza pale utakapohitajika.

