KONGAMANO LA KITAIFA LA USHIRIKI WA WATANZANIA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI NA UWEKEZAJI LAFANA
Imewekwa: 02 Sep, 2026
KONGAMANO LA KITAIFA LA USHIRIKI WA WATANZANIA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI NA UWEKEZAJI LAFANA

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uweeshaji Kiuchumi (NEEC) Bw. Gwakisa Bapala ametoa wito kwa Wadau wote walioshiriki katika Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji kushiriki katika Miradi ya Kimkakati kwani inasaidia kuinua Uchumi wa Taifa.

Ameyasema hayo hii leo September 2, 2026 katika Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji iliyofanyika katika Ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

“Kupitia kongamano hiili mtanufaika na fursa mbalimbali kwani utapata nafasi ya kukutana na wadau mbalimbali kutoka Taasisi mbalimbali watakaowasaidia kutupatia fursa za kiuchumi zitakazotusaidia katika kuinua Uchumi wa Mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla” aliongeza Bw. Gwakisa.

Aidha Bw. Gwakisa ameshukuru Taasisi zote za Umma na Binafsi walioshiriki katika kongamano hilo ambalo limeandaliwa na NEEC kwa kushirikiana na PURA, TPDC na kudhaminiwa na benki ya CRDB.

Katika Kongamano hilo mawasilisho kadhaa yalifanyika na kujadiliwa na wajumbe waliohudhuria lengo likiwa ni kuzifahamu fursa mbali mbali zinazopatikana nchini ambazo zinaweza kumsaidia Mtanzania.

Kongamano hilo litaendelea hadi taree 3 ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mb). Matarajio ya wengi ni kuweza kunufaika na Kongamano hilo na hatimaye kuinuka kiuchumi yeye binafsi na Taifa kwa ujumla.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo

slot gacor