Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu Dkt. James Henry Kilabuko azindua Mwongozo wa Kitaifa wa Uendelezaji wa vituo vya Biashara katika ukumbi wa hoteli ya Morena Mkoani Dodoma. Mwongozo huo umeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na kudhaminiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).
Akizindua Mwongozo huo Naibu Katibu Mkuu alisema umelenga kuboresha huduma zinazotolewa na wafanyabiasharaili kusaidia ukuaji wa Uchumi kupitia Mfumo bora wa huduma ambazo zitawasaidia wafanyabiashara.
Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi. Beng'i Issa alisema kuwa "Sisi kama Baraza tunaamini kuwa maendeleo ya Mjasiriamali na Mfanyabiashara ndio injini ya mageuzi ya kiuchumi, Ajira na Ustawi wa Wananchi. Vile vile Mwongozo huu umendaliwa kwa njia shirikishi kwa wadau wote.
Katibu Mtendaji aliwashukuru Benki ya Maendeleo Afrika kwa udhamini wao pamoja na wadau wote walioshiriki kuandaa nyenzo hiyo.

