Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Vipi vigezo vya kuwezeshwa kupitia Mfuko wa Uwezeshaji Mwananchi?

  • MEF inatoa na kukopesha fedha kwa njia ya dhamana au bila dhamana kwa wanaostahili ikijumuisha mtu mmoja mmoja,SACCOS, biashara za ubia, makampuni, mashirika na vyama vya ushirika.1.Baraza linawezesha vipi vijana

MEF ni moja ya mifuko ya Uwezeshaji iliyotajwa katika sera ya uwezeshaji wananchi ya mwaka 2004 ambayo inatumiwa na Serikali kusaidia utekelezaji wa jitihada mbalimbali za uwezeshaji wananchi Kiuchumi.MEF hasa husaidia kuondoa vikwazo vya mitaji na mikopo na kukuza mafunzo ya ujasiriamali.

Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi unafanyika katika njia mbalimbali ikiwemo mikopo,ruzuku,dhamana za mikopo,elimu kwa wazalishaji mali,taarifa za masoko na kutatua changamoto ambazo zimekuwa kikwazo katika kuinua uchumi wa wananchi.

Baraza linasimamia utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi na kuyafikia makundi yote ya uzalishaji mali wakiwemo wanawake, vijana na wazee kutoka kada zote.

  • Baraza linaratibu utekelezaji wa sera ya uwezeshaji kupitia madawati ya uwezeshaji yaliyopo kwenye Wizara, Mikoa na Halmashauri zote.II.Kupitia mikutano na wadau wa uwezeshaji katika kutathmini matokeo ya utekelezajki wa sera, mikakati na miongozo yake.
  • III.Kupitia majadiliano ya kushirikisha uzoefu na kupima matokeo ya shughuli za uwezeshaji.
  • Kuhimiza uwasilishaji wa ripoti kwa taasisi, wizara na sekta binafsi ili kupima matokeo ya uwezeshaji kwa Taifa.
  • Kutoa miongozo mbalimbali ya uwezeshaji kwa wadau

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ni chombo cha juu cha Serikali ambacho kinawajibika katika kusimamia,kufuatilia na kuratibu utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004