Ushiriki wa Watanzania

Imewekwa: May, 20 2019

Uratibu wa Ushiriki wa Watanzania Kwenye Uwekezaji

Uratibu wa Ushiriki wa Watanzania Kwenye Uwekezaji

Nchi ya Tanzania kwa sasa inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inatarajiwa kuipeleka nchi katika uchumi wa kati ifikapo 2025. Sanjari na hili, Serikali pia inatekeleza Sera ya Viwanda kupitia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (5) 2016/17 – 2020/21 kwa lengo la kuongeza pato la Taifa.

Utekelezaji wa masuala ya local content nchini Tanzania ni mtambuka unaogusa wadau wa sekta mbalimbali za kiuchumi. Miongoni mwa wadau hao ni pamoja na sekta ya umma (kupitia Wizara, Idara na Wakala wa Serikali), sekta binafsi (kupitia wawekezaji, wakandarasi, n.k). Kwa kuwa masuala ya local content ni mtambuka yanayoweka hitaji la umuhimu wa uratibu ili kuwezesha upatikanaji na upimaji wa taarifa za utekelezaji za ushiriki wa wananchi na makampuni ya watanzania katika miradi ya uwekezaji na ile ya kimkakati. Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ina jukumu la kuratibu, kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa masuala ya local content katika ngazi ya kitaifa kupitia sekta zote za vipaumbele kwenye kuzingatia masuala mbalimbali kama vile.

  1. Upatikanaji wa ajira na uendelezaji wa nguvukazi ya wananchi wa Tanzania
  2. Mpango wa urithishaji ujuzi na teknolojia
  3. Kuhakikisha kunakuwepo na ubia kati ya makampuni ya Tanzania na wawekezaji ili thamani ya ziada iweze kubaki nchinina Taifa kunufaika na fursa hizo
  4. Uendelezaji wa watoa huduma wa kitanzania na ununuzi wa bidhaa/malighafi zilizopo nchini
  5. Ushiriki wa jamii n.k

Uratibu unaofanyika unawezesha Serikali kutambua jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau hali inayoongeza chachu kwa Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuhakikisha masuala ya local content yanazingiwa katika hatua za awali kabla, wakati na baada ya utekelezaji na upimaji wa masuala ya local content. Uratibu unawezesha kuishauri Serikali kwenye mambo mbalimbali ambayo huleta faida za ustawi na maendeleo ya Taifa. Kuwepo kwa uratibu kumesaidia kuongeza ufahamu wa hali halisi, fursa, changamoto na mafanikio ya utekelezaji wa masuala ya local content katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

Baraza limeendelea na linaendelea kuratibu mikutano, warsha, makongamano mbalimbali ya wadau wa kamati za kisekta. Baraza limeunda kamati kwa lengo la kufahamu hali halisi ya utekelezaji wa sekta, kujadili na kushauriana kuhusu hatua za makusudi zinazopaswa kufanyiwa kazi na kuishauri Serikali mambo ya msingi yenye kuleta matokeo makubwa kwa wananchi wake. Mbali na hayo, Baraza pia limeweka utaratibu wa kuratibu vikao vya kamati za wataalam (national multi-sector local content technical committee) ambayo kimsingi hupitia taarifa mbalimbali zinazowasilishwa pamoja na mambo mengine. Kamati hii huongozwa na Mwenyekiti ambaye huwa ni Katibu Mtendaji wa NEEC na kamati ya uongozi (National Steering Committee for Entrepreneurship Development) pamoja na kujadili masuala ya ujasiriamali hupitia masuala ya local content na Mwenyekiti wa kamati hii huwa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu).

Sanjari na hayo, kuna jumla ya waratibu wapatao 58 kutoka katika Wizara (26), Taasisi za Serikali (31) na mwamvuli wa sekta ya umma - TPSF (1) ambao huwa na jukumu la kuhudhuria vikao na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kupitia ofisi wanazokotoka.

Uratibu wa Ushiriki wa Watanzania Kwenye Uwekezaji