Karibu

Karibu kwenye tovuti ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC). NEEC ilianzishwa mwaka 2005 ili kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004. Katika mwaka huo huo Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ilianzishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuipa nguvu ya kisheria utekelezaji wa Sera. Tovuti hii inatoa maelezo ya kina kuhusu NEEC, kazi zake muhimu, nguzo na fursa za uwezeshaji, programu za ushirikiano na miradi, na inatoa kiunganishi na tovuti nyingine husika. Tunathamini ushiriki wako katika kufungua na kusoma tovuti na iwapo una swali lolote / maoni / ushauri unaweza kutuma kupitia anwani iliyooneshwa katika ukurasa wa "wasiliana nasi".